1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Jeshi la Israel lauwa Wapalestina 4 Ukingo wa Magharibi

3 Julai 2023

Jeshi la Israeli limesema limefanya mashambulizi ya kutumia ndege zisizo na rubani leo kwenye mji wa Jenin huko Ukingo wa Magharibi. Wizara ya Afya ya Palestina imearifu vifo vya watu watano na wengine 27 walijeruhiwa.

Westjordanland Region Dschenin | Israelische Militäroperation | Palästinensische Jugendliche
Picha: Jaafar Ashtiyeh/AFP/Getty Images

Kulingana na mkuu wa Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina Mahmoud al-Saadi mji wa Jenin umelengwa kwa makombora kutoka angani na uvamizi wa vikosi vya ardhini vya Israel. Afisa huyo amekaririwa akisema nyumba kadhaa zimeshambuliwa na moshi unafuka kutoka kila sehemu ya mji huo.

Jeshi la Israeli limezitaja hujuma hizo kuwa ni sehemu ya operesheni ya kupambana na ugaidi na imeyalenga maeneo yanayotumika na makundi ya wanamgambo kuhifadhi silaha na kupanga mashambulizi.

Soma pia: Israel yafanya operesheni kubwa ya kijeshi mjini Jenin

Operesheni hiyo imefanyika kiasi wiki mbili tangu jeshi la Israel lilipoivamia kambi ya wakimbizi ya mji wa Jenin na kuwauwa watu 7.