1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia maeneo ya Hezbollah nchini Lebanon

30 Oktoba 2024

Jeshi la anga la Israel limeyashambulia maeneo zaidi ya 100 ya Hezbollah nchini Lebanon katika kipindi cha siku moja.

Shambulio la Israel dhidi ya miundombinu ya Hezbollah nchini Lebanon
Shambulio la Israel dhidi ya miundombinu ya Hezbollah nchini Lebanon.Picha: KAWNAT HAJU/AFP

Jeshi la Israel pia limesema limewaua wapiganaji kadhaa wa kundi hilo, huku wanajeshi wake wakiendelea na uvamizi katika maeneo kadhaa ya Hezbollah kusini mwa Lebanon.

Wanajeshi wa Israel wamegundua shehena kubwa za silaha, kuharibu mahandaki, kuwaangamiza magaidi na kuharibu mitambo ya kurushia makombora ya Hezbollah iliyokuwa imefichwa katika maeneo ya umma na yaliyolenga kuzishambulia jamii za Waisraeli.

Soma pia:Hezbollah yamtangaza Naim Qassem kuwa kiongozi mpya 

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Lebanon, raia kadhaa waliuwawa katika mashambulizi ya Israel. Jeshi la Israel pia limeendelea na operesheni yake kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW