MigogoroAfrika
Jeshi la Kongo lakamata silaha za kijeshi Ituri
6 Machi 2026
Matangazo
Msemaji wa jeshi la Kongo kwenye jimbo hilo, Jules Ngongo amesema miongoni mwa silaha zilizokamatwa ni pamoja na bunduki za rashasha chapa AK47, maroketi na kasha nyingi za risasi.
"Oneni wenyewe silaha na risasi tulizokamata. Walikuwa wamezificha ili kuua raia wa Ituri. Jeshi tumekuwa tukifanya kazi hii kuhakikisha amani inarejea kote nchini na tutakwenda hatua kwa hatua hadi turejeshe usalama wa taifa", amesema afisa huyo wa jeshi wakati wa msako.
Jeshi hili linashuku silaha hizo ni mali ya kundi la Convention pour la Révolution Populaire (CRP) linaloongozwa na Thomas Lubanga, ambaye hivi karibuni alitangaza kuungana na waasi wa M23.