1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Kongo lashambulia waasi

Admin.WagnerD17 Julai 2013

Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa kutumia helikopta yameyashambulia maeneo ya waasi karibu na upande wa mashariki mwa mji wa Goma, ikiwa siku ya tatu ya mapigano makali yaliyosabaisha wimbi la ukimbizi.

A Congolese army soldier walks through the bush, back from an attack position north-west of Munigi, overlooking the front-line, in the east of the Democratic Republic of the Congo on July 15, 2013. Fighting broke out yesterday between M23 rebels and the national army, and continued today, with heavy artillery fire north-west of Munigi and the army claiming to have taken ground. AFP PHOTO/PHIL MOORE (Photo credit should read PHIL MOORE/AFP/Getty Images)
Kämpfe im OstkongoPicha: Phil Moore/AFP/Getty Images

Katika barua ilitumwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambayo Shirila la habari la Reuters limepata nakala yake, Kongo imekituhumu kikosi maalumu cha Rwanda kwa kuwasaidia waasi wa M23 katika mapigano hayo. Lakini pia katika taarifa yao walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo wamekanusha madai ya Rwanda kwamba walifyatua makombora dhidi ya nchi hiyo kutoka ardhi ya Kongo Jumatatu.

Taarifa ya jeshi hilo la ulinzi wa amani lijulikalo kama MONUSCO, umesema wanajeshi wake hawajahusika na mapigano katika eneo la Goma na kwa hivyo hawawezi kuhusika katika kufyatua makombora kwenye mipaka ya Rwanda.

Malalamiko ya Rwanda

Katika taarifa tofauti iliyotolewa jumatatu kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Rwanda imelituhumu jeshi maalumu la ulinzi wa amani nchini Kongo kuwa linashirikiana na waasi wa Kihutu, wa kundi la FDLR, ambao wanahusishwa na mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994. Jeshi hilo jipya lina mamlaka ya kupigana na kuwanyang'anya silaha waasi katika eneo la mashariki mwa Kongo.

Rais Paul Kagame wa RwandaPicha: Reuters

Mpaka sasa walinzi hao wa amani 3,000 kutoka Afrika Kusini, Tanzania na Malawi wanafanya doria lakini bado hawajajiingiza katika mapigano. Umoja wa Mataifa tayari umekwisha onya, kwamba utazuia shambulio lolote lenye kulenga Goma, mji wenye kiasi ya watu milioni moja, ambao mwezi Novemba ulitekwa na waasi kwa kipindi kifupi.

Mwandishi wa Reuters katika eneo la Mutaho, kiasi cha kilometa saba, kaskazini/mashariki mwa Goma amesema aliziona helikopta tatu za jeshi la Kongo zikishambulia eneo la waasi, mji wa Kibati ambao upo umbali ya kilometa 4 zaidi.

Eneo la Munigi, pembezoni mwa mji wa GomaPicha: Phil Moore/AFP/Getty Images

Msemaji wa Jeshi Kanali Olivier Hamuli aliliambia shirika hilo mjini Mutaho, kwamba hali hivi sasa imetulia. Akizungumzia operesheni ya asubuhi ya jana amesema walishambulia jana alfajiri lakini walijibu mapigo na kwamba lengo lao ni kuwasafisha waasi wote wa M23.

Awali Jumatatu Waasi na Majeshi ya Kongo walifyatuliana makombora karibu na kaskazini na magharibi mwa viunga vya mji wa Goma. Umoja wa mataifa unasema makombora hayo yalifika umbali wa mita 100 kutoka uwanja wa ndege wa Goma lakini hakuna hasara zozote zilizoripotiwa.

Mwandishi: Sudi Mnette RTR
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW