1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

Jeshi la Kongo lavunja mahusiano na wapiganaji wa FDLR

22 Novemba 2023

Mapigano makali yameibuka tena katika mji wa Kitshanga wilayanii Masisi kivu kaskazini kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23, huku Marekani ikitangaza Kongo na Rwanda zimekubaliana juu ya hatua za kupunguza mzozo.

Kongo I Wapiganaji wa FDLR
Mzozo | Wapiganaji wa kundi la FDLR wakilinda doriaPicha: Ricky Gare/dpa/picture alliance

Mapigano hayo yanaendelea wakati jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo limewataka maafisa wa jeshi kuvunja ushirikiano wote na kundi la wapiganaji wa FDLR wanaoendesha harakati zao katika sehemu mbalimbali katika eneo la kivu kaskazini.

Katika tangazo hilo lililotolewa kupitia msemaji wake Sylvain EKENGE, jeshi limetishia kuwafikisha mahakamani mafisa wote wa kijeshi atakayejenga ushirikano na kundi hilo lenye mizizi yake nchini Rwanda.

Vyanzo vya ndani vimeeleza kuwa milio ya silaha nzito na nyepesi ilisikika siku nzima ya jana karibu na mji wa Kitshanga ambako hali ya wasiwasi iliwalazimisha mamia ya raia kukimbia makazi yao baada yakushuhudiwa kwa vifo vya watu na wengine kadhaa kujeruhiwa katika kijiji kidogo cha Ndondo.

Soma pia:M23 wakiteka tena kijiji cha Kishishe mashariki mwa Kongo

Licha yakuanza kurejea kwa hali ya utulivu kwenye eneo hilo lililoshuhudia machafuko hayo ,leo asubuhi siku ya Jumatano raia waliopata hifadhi   kwenye kambi ya jeshi la walinda amani wa Umoja wa Mataifa ,wamezuiliwa kurejea majumbani kwao huku shughuli mbalimbali zikiwa zimekwama.

M23 yaongeza kasi ya mashambulizi

Tangu mwishoni mwa mwezi wa septemba,waasi hao wa M23 wanaodaiwa kusaidiwa na jeshi la Rwanda, wameongeza kasi ya kuvishambulia vijiji wanavyodai kutawaliwa na makundi ya wapiaganaji ikiwemo waasi wa kihutu kutoka Rwanda ,FDLR madai ambayo jeshi la Congo limekuwa likikanusha kwa mara kadhaa.

Vita vya M23 vinaathiri pia wakazi wa Bukavu

02:40

This browser does not support the video element.

Ikuku ya Marekani White House, ilisema jana kwamba mkuu wa intelijensia wa Marekani Avril Haines amepata uhakikisho kutoka marais wa Rwanda, Paul Kagame, na mwenzake wa Kongo Felix Tshisekedi juu ya kupunguza uhasama baina ya mataifa hayo mawili, alipozuru mataifa hayo siku ya Jumapili na Jumatatu.

Soma pia:Jeshi la Congo, askari wa UN watangaza operesheni ya pamoja dhidi ya waasi wa M23

White House imesema Marais Paul Kagame na Felix Tshisekedi, kila moja wao alitoa ahadi ya kuounguza mzozo mashariki mwa Kongo, na kuongeza kuwa Marekani itafuatilia juhudi zao.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW