1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Jeshi la Mali lapambana na waasi karibu na mji wa Kidal

Sylvia Mwehozi
13 Novemba 2023

Mapigano yalizuka tena jana Jumapili kati ya jeshi na makundi yanayotaka kujitenga ya Tuareg na waasi, huko kaskazini mwa Mali kwa mujibu wa pande zote mbili.

Waasi wa Mali
Wapiganaji kutoka vuguvugu la ukombozi wa Azawad huko MaliPicha: Souleymane Ag Anara/AFP

Mapigano yalizuka tena jana Jumapili kati ya jeshi na makundi yanayotaka kujitenga ya Tuareg na waasi, huko kaskazini mwa Mali kwa mujibu wa pande zote mbili.

Soma pia: Jeshi la Mali lapeleka jeshi kaskazini kupambana na waasi

Jeshi la Mali, lilisema kuwa limepata mafanikio makubwa kutokana na matumizi ya rasilimali za anga na ardhi. Nao muungano wa makundi yenye silaha ya Tuareg, ulidai kuwakamata wanajeshi wa Mali na mamluki kutoka kundi la Wagner la Urusi katika eneo lililoko kilometa 25 kutoka mji wa Kidal.

Tangu walipotwaa mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2020, watawala wa kijeshi wa nchi hiyo wamedhamiria kurejesha mamlaka na utulivu katika mikoa yote. Hata hivyo mkoa wa Kidal unaonekana kuwa uwanja muhimu wa vita.

Kuondolewa kwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani kutoka Mali kumeongeza hali ya ukosefu wa utulivu.