1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Jeshi la Marekani ladungua droni na makombora ya Wahouthi

Saleh Mwanamilongo
2 Juni 2024

Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani CENTCOM imesema hakuna majeraha au uharibifu ulioripotiwa na meli yoyote katika njia ya biashara yenye shughuli nyingi baada ya matukio hayo.

Jeshi la Marekani ladungua droni na makombora ya Wahuthi katika Bahari ya Shamu
Jeshi la Marekani ladungua droni na makombora ya Wahuthi katika Bahari ya ShamuPicha: Chris Sellars/AP Photo/MoD Crown/picture alliance

Jeshi la Marekani limesema limedungua droni na makombora mawili yaliyorushwa na waasi wa Houthi wa Yemen kusini mwa Bahari ya Shamu. Taarifa ya jeshi imesema mabomu hayo yaliangushwa Jumamosi katika matukio mawili tofauti.

Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani CENTCOM imesema hakuna majeraha au uharibifu ulioripotiwa na meli yoyote katika njia ya biashara yenye shughuli nyingi baada ya matukio hayo.

Waasi wa Houthi, ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya Yemen, wamefanya mashambulizi ya droni na makombora katika eneo hilo tangu Novemba. Wakielezea mashambulizi yao kama kitendo cha kulipiza kisasi vita vya Israel na Hamas.

Mashambulizi hayo ya waasi yamesababisha hatua ya ulipizaji kisasi ya vikosi vya Marekani na Uingereza na kuunda muungano wa kimataifa kulinda njia muhimu za meli kupitia Ghuba ya Aden na Bahari ya Shamu.