1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Jeshi la Marekani lashambulia nchini Syria na kuua watu 10

24 Machi 2023

Jeshi la Marekani jana lilifanya mashambulizi dhidi ya wapiganaji wanaofungamana na jeshi la ulinzi wa kimapinduzi la Iran, IRGC, mashariki mwa Syria.

Autonome Waffen | Kamikaze-Drohne
Picha: AeroVironment, Inc/abaca/picture alliance

Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Marekani, hatua hiyo imechukuliwa baada ya kutokea shambulizi lililofanywa kwa kutumia ndege isiyoendeshwa na rubani nchini Syria na kumuua mkandarasi mmoja wa Marekani na wengine sita kujeruhiwa.

Soma pia: Mashambulizi ya Marekani Syria yadaiwa kuwajeruhi raia kadhaa

Wizara ya ulinzi imesema shambulizi hilo lilifanywa dhidi ya kituo cha shughuli za ukarabati katika kambi ya vikosi vya muungano karibu na mji wa al Haskákah, kaskazini mashariki mwa Syria. Ndege iliyofanya shambulio hilo imetajwa kuwa ya Iran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW