1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Jeshi la Myanmar liliagiza silaha kukiuka haki za binadamu

18 Mei 2023

Myanmar iliagiza silaha zenye thamani ya dola bilioni moja tangu ilipokamata madaraka kupitia mapinduzi mwaka 2021 na inatumia silaha hizo kufanya ukatili.

Myanmar | Militär
Picha: AFP/Getty Images

Kulingana na ripoti hiyo ya mtaalamu wa Umoja wa Mataifa,iliyotolewa jana, jeshi la Myanmar liliagiza silaha na vifaa kutoka Urusi zenye thamani ya dola milioni 406, na kutoka China, silaha zenye thamani yad ola milioni 267.

Kampuni za India pia zililiuzia jeshi la Myanmar vifaa vya thamani yad ola milioni 51.

Myanmar imekuwa ikizongwa na machafuko tangu mapinduzi hayo, ikiwemo mapigano mapya ya kikabila kati ya makundi ya waasi na makumi ya vikosi vya sungusungu "People's Defence Forces” dhidi ya jeshi.

Ripoti imesema jeshi limewaua zaidi ya watu 3,500 katika ukandamizaji wake dhidi ya upinzani, na kwamba idadi ya wafungwa wa kisiasa imeongezeka hadi 20,000.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW