UgaidiNiger
Jeshi la Niger ladai kumuua mwanachama muhimu wa kundi la IS
24 Juni 2024Matangazo
Makabiliano hayo yalifanyika magharibi mwa nchi hiyo katika eneo lisilo na utulivu la Tillaberi kunakopatikana mipaka ya nchi tatu za Niger, Mali na Burkina Faso ambako kwa miaka kadhaa sasa, magaidi wamekuwa wakifanya mashambulizi licha ya kutumwa kwa vikosi vya usalama.
Soma pia: Watu 5 wameuwawa kwenye shambulio la itikadi kali Niger
Jeshi pia limesema pia kuwa siku ya Alhamisi magaidi tisa waliuawa na wengine 31 walikamatwa katika operesheni ya kupambana na makundi ya jihadi katika eneo hilo.