1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Pakistan yaanzisha operesheni dhidi ya waasi wa Balochistan

30 Agosti 2024

Jeshi la Pakistan limeanzisha operesheni ya kijasusi katika jimbo la kusini magharib la Balochistan, kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo na kuwaua zaidi ya watu 50 wiki hii.

Pakistan | Moshi ukifuka kwenye moja ya mitaa mashuhuri.
Moshi ukifuka angani kufuatia mlipuko.Picha: Karim Ullah/AFP

Taarifa ya jeshi hilo imesema waasi watano waliuawa na watatu walijeruhiwa katika operesheni tatu ilizozianzisha kwenye jimbo hilo.

Imesema, operesheni hizo zitaendelea hadi washambuliaji, wafadhili na washirika wao kwenye matukio hayo mabaya kabisa watakapofikishwa mbele ya sheria.

Soma pia:Idadi waliouawa mashambulizi ya Pakistan yafikia 39

Waasi wa kabila ya Baloch mapema wiki hii walishambulia baadhi ya vituo vya kijeshi na kiraia katika msururu wa mashambulizi ya kupangwa, huku Kundi la Baloch Liberation Army, likikiri kuhusika.