SiasaAsia
Jeshi la Pakistan lawaua wanamgambo 30
20 Novemba 2025
Matangazo
Jeshi la Pakistan limesema hayo Alhamisi baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kuwaua watu 12 wiki iliyopita mjini Islamabad.
Wanamgambo 23 waliuawa katika mashambulizi ya wilaya ya Kurram kwenye jimbo la Khyber Pakhtunkhwa jana.
Katika taarifa iliyofuata, jeshi limesema wanamgambo wengine saba waliuawa katika operesheni tatu tofauti kwenye wilaya za Mohmand, Lakki Marwat na Tank Novemba 18 na 19.
Mapambano dhidi ya wanamgambo kuendelea
Jeshi limesema Pakistan itaendelea kupambana na kuondoa kitisho cha ugaidi unaofadhiliwa na kuungwa mkono na mataifa ya kigeni.
Mara kwa Mara Pakistan imekuwa ikiishutumu nchi jirani ya Afghanistan kwa kuyahifadhi makundi ya wanamgambo, na hasa kundi la Tehreek-e-Taliban, TTP, ambalo hufanya mashambulizi nchini Pakistan.