1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Jeshi la Somalia latwaa udhibiti Jimbo la Kusini Magharibi

31 Machi 2026

Jeshi la Somalia limetwaa udhibiti wa jimbo la Kusini Magharibi, hatua iliyomfanya rais wa jimbo hilo kujiuzulu wiki mbili baada ya serikali yake kusema ilikuwa inavunja mahusiano na serikali kuu mjini Mogadishu.

Somalia Baidoa Mogadishu
Kikosi cha Walinda Amani wa Umoja wa Afrika katika eneo la Baidoa, Kusini Magharibi mwa Somalia.Picha: Ed Ram/Getty Images

Wanajeshi wa Somalia waliripotiwa kuingia kwenye mji mkuu wa jimbo hilo, Baidoa, siku ya Jumatatu (Machi 30).

Baidoa ni wa kimkakati wenye makao makuu ya kikosi cha kimataifa wa walinda amani na mashirika kadhaa ya kibinaadamu, kwenye eneo hilo lililoathirika kwa ukame, migogoro na wakimbizi wa ndani.

Rais wa jimbo hilo, Abdiaziz Hassan Mohamed Laftagareen, aliandika kupitia mtandao wa Facebook kuwa amejiuzulu wadhifa wake, siku chache baada ya kuchaguliwa kuongoza tena kwa muhula mwengine wa miaka mitano.

Wakaazi wengi wameukimbia mji wa Baidoa na baadhi ya mashirika ya misaada yamesitisha shughuli zao, wakihofia mapigano kati ya wanajeshi wa serikali kuu na vikosi vya jimbo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW