Jeshi la Somalia lawauwa al-Shabba 16, kuwakomboa watoto 40
28 Septemba 2020Kamanda mwandamizi wa jeshi la Somalia Ahmed Hassan amesema watoto hao walitekwa nyara na kundi hilo kama sehemu ya uwezekano wa kuwatumia kama wapiganaji baadae.
Wanajeshi hao walikikomboa kijiji cha Nuunay ambako kundi hilo la wanamgambo lilikuwa likiwashikilia watoto takriban 40 ambao walipanga kuwatumia kama washambuliaji wa kujitowa muhanga na wapiganaji wa siku za baadae. Watoto hao walikombolewa na jeshi hivi sasa linatarajia kuwarudisha kwa familia zao,kwa mujibu wa kamanda wa Jeshi.
Tukio hilo limeshuhudiwa siku ya Jumamosi. Kadhalika wanajeshi wa Somalia na Kenya walifyetuliana risasi kwa muda wa dakika kadhaa siku ya Jumamosi katika eneo la mpaka baina ya mataifa hayo mawili. Tukio hilo limefanyika baada ya jeshi la Kenya kufyetua risasi kuwazuia waandamanaji waliokuwa upande wa Somalia kuelekea upande wa Kenya.