1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Jeshi la Sudan Kusini lauteka tena mji wa Nasir

Saleh Mwanamilongo
21 Aprili 2025

Wanajeshi wa Sudan Kusini wametangaza kuuteka tena mji muhimu katika jimbo la Upper Nile ambao liliupoteza kufuatia mapigano na wanamgambo wa kabila la Nuer mwezi Machi.

Wanajeshi kutoka Sudan Kusini wanatua Goma kushiriki operesheni ya kulinda amani ya jumuiya ya EAC
Wanajeshi kutoka Sudan Kusini wanatua Goma kushiriki operesheni ya kulinda amani ya jumuiya ya EACPicha: Glody Murhabazi/AFP

Msemaji wa jeshi na yule wa wapiganaji wa kundi la White Army wamesema mji wa Nasir ulitekwa tena siku ya Jumapili bila mapigano.

Aidhaa, Honson Chuol James, msemaji wa kundi la White Army amesema watu 17 waliuawa katika mashambulizi makubwa ya mabomu katika kijiji jirani cha Thuluc. Akililaumu jeshi kuendesha mashambulizi hayo dhidi ya raia.

Kwa upande wake, msemaji wa jeshi Lul Ruai Koang amesema wanajeshi walizuia shambulizi la kuvizia la wapiganaji huko Thuluc.

Mapigano kati ya jeshi na wapiganaji wa kundi la White Army yalisababisha kukamatwa mjini Juba kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar na wanasiasa wengine kwa tuhuma za kuwaunga mkono waasi hao.