1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Jeshi la Sudan ladai kumuua kamanda mkuu wa RSF

14 Juni 2024

Jeshi la Sudan leo Ijumaa limedai kumuua kamanda mkuu wa jeshi la wanamgamno wa RSF, Ali Yagoub Gibril, wakati wa mapambano katika mji wa Al-Fashir kaskazini mwa Darfur.

Sudan | Wanamgambo wa RSF
Vikosi vya wanamgambo wa RSF Picha: Mohamed Babiker/Photoshot/picture alliance

Yagoub Gibril alikuwa kamanda mkuu wa RSF huko al-Fashir, mji mkuu wa mwisho katika mkoa wa Darfur nchini Sudan eneo pekee ambalo halijadhibitiwa na wanamgambo wa RSF.

Hata hivyo RSF haijatoa maoni kuhusiana na madai hayo.

Soma pia: UN yataka mzingiro wa kijeshi wa El-Fasher Darfur ukomeshwe

RSF imekuwa ikizingira mji wa al-Fashir, wenye wakaazi milioni 1.8, kwa wiki kadhaa.

Maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa wameonya kwamba mzozo unaozidi kukua unaweza kusababisha kuenea kwa vita vya kijamii.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW