Jeshi la Sudan laendelea kufunga anga
31 Julai 2023Matangazo
Anga la Sudan lilifungwa kwa safari za kawaida za ndege baada ya kuzuka mgogoro wa kijeshi kati ya jeshi la nchi hiyo na vikosi vya wanamgambo wa RSF katikati ya Aprili.
Kwingineko, wanamgambo wa RSF waliwaamuru raia kuyahama makaazi yao kusini mwa mji mkuu Khartoum.
Soma zaidi: Mjumbe wa RSF asema ni wakati wa amani Sudan, Darfur
Wakaazi kadhaa walisema kuwa wanamgambo hao waliwaambia walikuwa na masaa 24 kuyahama makaazi yao.
Mamia ya wakaazi wanafurushwa kutoka kitongoji cha Jabra kilichopo kusini mwa Kahrtoum, ambako pamoja na eneo jirani la Sahafa ni makao ya jeshi la Sudan pamoja na kituo cha RSF kinachotumiwa na jenerali wa wanamgambo hao, Mohamed Hamdan Dagalo.