1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Sudan lapambana na wanamgambo Port Sudan

19 Septemba 2023

Mashahidi wanasema mapigano yamezuka katika hilo la pwani la Port Sudan kati ya wanajeshi na wanamgambo wa kikabila yakiwa ya kwanza kwenye eneo hilo tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan mnamo mwezi Aprili.

Sudan Unruhe Konflikt
Picha: AFP via Getty Images

Kwa mujibu wa mashahidi hao, kulikuwa na ufyatulianaji wa risasi kati ya jeshi na kundi la wanamgambo linaloongozwa na Sheba Darar, kiongozi kutoka kabila la Beja, katikati ya jimbo hilo.

Soma: Jenerali wa juu wa Sudan amshutumu mpinzani wake kwa uhalifu na kuwadanganya raia

Port Sudan ndipo ulipo uwanja wa ndege pekee unaofanya kazi na maafisa wa serikali na Umoja wa Mataifa wanaishi hapo baada ya kuhama kutoka kwenye mji mkuu wa Sudan, Khartoum, ambao umegubikwa na vita.

Hadi mapigano hayo ya usiku wa Jumatatu (Septemba 18) jimbo hilo lilikuwa halijawahi kukumbwa na ghasia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW