1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Jeshi la Sudan, raia wakubaliana kumaliza mzozo

5 Desemba 2022

Watawala wa kijeshi nchini Sudan na viongozi wa kiraia wametia saini hii leo makubaliano ya awali ya kumaliza mzozo mkubwa wa kisiasa unaoiandama nchi hiyo ya Afrika tangu kutokea mapinduzi ya jeshi mwaka mmoja uliopita.

Sudan Khartoum | Abkommensunterzeichnung - Abdel Fattah al-Burhan
Picha: AFP via Getty Images

Mkataba huo wa leo umesainiwa na mkuu wa utawala wa kijeshi  Abdel Fattah al-Burhan, kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia cha RSF,  Mohamed Hamdan Dagalo, na wawakilishi wa makundi kadhaa ya kiraia ikiwemo yaliyoondolewa wakati wa mapinduzi ya mwaka jana.

Makubaliano hayo yanaweka msingi wa kuundwa kwa serikali ya mpito ya kiraia na yatafuatiwa na majadiliano mapana juu ya masuala mengine muhimu ikiwemo uendeshaji uchumi na usimamizi wa fedha za umma.

Kutiwa saini makubaliano hayo kunafungua njia za kuirejesha Sudan chini ya utawala wa kiraia ulioparaganyika mwaka jana baada ya jeshi kuchukua madaraka kwa nguvu.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa walioshiriki kwenye mazungumzo hayo ya Ijumaa, ingawa hapo jana waandamanaji wanaopinga mpango huo waliandamana nje ya ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Khartoum wakisema hawataki masuala ya ndani ya nchi yao yaingiliwe na Umoja huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW