1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria ilitumia gesi za kemikali kushambulia wapinzani - OPCW

27 Januari 2023

Uchunguzi uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Silaha za Kemikali (OPCW) umebaini kuwa jeshi la anga la Syria lilidondosha mitungi miwili iliyokuwa na gesi ya chlorine katika mji wa Douma Aprili, 2018.

Syrien Wahl 2021 | Bashar al Assad
Picha: Syrian Presidency Facebook page/AFP

Watu 43 waliauwa katika shambullizi hilo.

Ripoti ya shirika hilo iliyotolewa leo, imethibitisha kuwa utawala wa Rais Bashar Al-Assad ulitumia silaha za kemikali wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

Mkurugenzi Mkuu wa OPCW, Fernando Arias, amesema matumizi ya silaha za kemikali Douma na kwengineko hayakubaliki na yanakiuka sheria za kimataifa.

Syria ambayo ilijiunga na OPCW mwaka 2013 kutokana na shinikizo la jumuia ya kimataifa baada ya kulaumiwa kwa shambulizi jengine la silaha za kemikali, haitambui mamlaka ya timu ya uchunguzi na mara kwa mara imekana kutumia silaha za kemikali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW