Ujerumani kuendelea na UNMISS na Sea Guardian Sudan Kusini
25 Januari 2024Msemaji wa serikali ya ujerumani Steffen Hebestreit, amesema Jumatano mjini Berlin kwamba baraza la mawaziri nchini humo, limeidhinisha kuongezwa kwa muda wa kuhudumu wa misheni zote mbili hadi Machi 2025.
Shughuli zinazofanywa na misheni ya Sea Guardian na UNMISS
Sea Guardian hutumia meli na ndege kufuatilia shughuli katika bahari ya Mediterenia na inatarajiwa kukabiliana na ugaidi na kuingizwa kwa silaha haramu.
Soma pia: 2023: Mwaka wa changamoto kwa walinda amani wa UN Afrika
UNMISS iliibuka kutoka kwa misheni iliyotangulia UNMIS kwa kutangazwa uhuru na Sudan Kusini mnamo mwaka 2011 na inakusudiwa kusaidia katika mchakato wa amani na kulinda raia.
Bunge la Ujerumani Bundestag bado linapaswa kuamua kuhusu muda wa kuongezwa kwa operesheni hizo.