1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JESHI LA UJERUMANI KUTUMIKA LEBANON

20 Septemba 2006

Bunge la Ujerumani limeidhinisha kutumwa kwa kikosi cha wanamaji wa Ujerumani kulinda mwambao wa Lebanon.Mada hii na machafuko nchini hungary kudai waziri mkuu ajiuzulu kwa kuwa alisema uwongo zimechambuliwa kwa mapana na marefu.

Waziri mkuu wa hungary ajiuzulu-dai la wapinzani.
Waziri mkuu wa hungary ajiuzulu-dai la wapinzani.Picha: AP

Tukianza na gazeti la WESTFÄLISCHE NACHRICHTEN laandika:

“wazi ni kuwa, Jeshi la Ujerumani-Bundeswehr- linahitaji mpumzi nyingi.Kwani, muda uliopewa jeshi hilo kulinda amani hadi August,mwakani hautoshi kabisa.Na hasa kwavile, jukumu hili linaambatana na hatari kubwa ,wale wanaolitilia shaka,wafaa kutolewa shaka shaka hizo.

Serikali ya Ujerumani ingeonesha busara ikiwa itatoa na mapema ishara wazi ya kisiasa .Yule anaelipeleka jeshi la Ujerumani Lebanon na kwengineko kwenye misukosuko, anabidi kuona jeshi hilo linapata fedha na zana za kutosha.” –ni maoni ya Westfälischen Nachrichten.

Gazeti la KIELER NACHRICHTEN linasema kuwa kwa mara ya kwanza majeshi ya Ujerumani yapelekwa Mashariki ya kati ambako jukumu na kumalizika kwake hakuonekani.Kikijikuta sasa upande wa upinzani, chama cha Kijani cha walinzi wa mazingira kingeweza kupinga kupelekwa kwa jeshi hilo.

Lakini, chama hiki kinahiyari kutopinga na kujipatia sifa za ukakamavu kama anazovuna Oskar Lafontaine wa (chama cha mrengo wa shoto) na Guido Westerwelle wa (chama cha kiliberali cha FDP)…

Kuhusu msimamo wa chama cha FDP katika mjadala bungeni,gazeti la kibiashara kutoka Düsseldorf,

Handelsblatt laandika:

“Mpaka wa kuonesha upumbavu ameukiuka mwenyekiti wa chama hicho cha FDP anaponadi kwamba kwanza lipatikane suluhisho la amani huko Mashariki ya kati,chuki zimalizike,ndipo yafaa kuzungumzia kutuma majeshi huko.Upumbavu wa kima kama hicho hafai mtu kuutarajia kutoka FDP.”

Gazeti la ABENDZEITUNG kutoka Münich lina maoni tofauti linapoandika:

“Mtu hajitosi tu kirahisi katika balaa la Lebanon,kwani jukumu hilo ni la kutia wasi wasi.Kwahivyo, maoni yanayopinga kujitosa huko yafaa kutiwa maanani na kusikilizwa na chama cha FDP hapo kinastahiki kupewa heko.”

Likitugeuzia mada na kutupia macho machafuko nchini Hungary, gazeti la WESTDEUTSCHE ALLGEMEINE ZEITUNG linalotoka mjini Essen laandika:

„ Picha tunazoziona zinasisimua.Mtu anakumbushwa uasi wa 1956 katika kudai waziri mkuu an’gatuke kwavile amesema uwongo katika kushinda uchaguzi.Demokrasia changa yahitaji wanasiasa wenye dhamana na sio wasema uwongo.Lakini nini alichofanya hasa waziri mkuu Gyurcsany ? Alijihukumu yeye na chama chake .

Na ilipofichuka siri ikazua balaa la machafuko haya.”

Gazeti la OSTSEE-ZEITUNG linalochapishwa mjini Rostock linatufunulia kawa juu ya tabia za uchaguzi linapoandika:

‘Hakuna uwongo mwingi unaotoka kama nyakati za kampeni za uchaguz, nyakati za vita na baada ya kuwinda’-aliwahi kusema hayo Otto von Bismark.

Kanzela huyo alietawala kwa mkono wa chuma hakukosea aliyosema kama kashfa ya hivi punde ya waziri mkuu wa chama cha kijamaa cha Hungary inavyothibitisha.

Wabunge na waakilishi wengi yadhihirika wanaamini yafaa kuwawaambia wapigakura kile wanachopenda kusikia.Na miongoni mwa hayo,kuwapa ahadi usizoweza kuwatimizia.”-uchambuzi wa OSTSEE-ZEITUNg kutoka Leipzig.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW