1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUjerumani

Jeshi la Germany lina utayari kubeba dhamana NATO?

10 Julai 2024

Viongozi wa Jumuia ya Kujihami ya NATO wanakutana mjini Washington, Marekani, ambako wanajadiliana mambo mbalimbali kuanzia kuiunga mkono zaidi Ukraine, changamoto za China katika mzozo wa Urusi na Ukraine.

Ukraine | Wanajeshi wa Ujerumani wakiwa na wenzao wa Ukraine
Wanajeshi wa Ujerumani wakiwa na wenzao wa UkrainePicha: Jens Büttner/dpa/picture alliance

NATO ilianzishwa kufanya kazi kama muungano wa kijeshi kujilinda dhidi ya Umoja wa Kisovieti. Ndani ya jeshi hilo, jeshi la Ujerumani Magharibi lilipata mafunzo ya kujilinda dhidi ya mashambulizi kutoka Ujerumani Mashariki. Miongo mitatu baadae, kitisho kinakuja tena kutoka Urusi. 

Ilikuwa mwanzoni mwa mwaka 1996, wakati wanajeshi wa Ujerumani wakiwa wamevalia nguo za kivita walipoingia kwenye eneo la nchi nyingine ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Wajerumani hawakwenda Bosnia-Herzegovina kama walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa, bali kama sehemu ya Kikosi cha Utekelezaji kinachoongozwa na NATO, cha IFOR.

Mnamo mwaka 1992, iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia ilitumbukia katika vita vilivyosababisha umwagaji damu zaidi katika ardhi ya Ulaya tangu mwaka 1945, na Warsebia walio wachache nchini humo, wakisaidiwa na majeshi ya kiongozi wa kibabe wa Serbia, Slobodan Milosevic.

Desemba mwaka 1995, pande zinazohasimiana, nchi jirani, na wakuu wa nchi na serikali za Marekani, Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani zilisaini Makubaliano ya Amani ya Dayton.

NATO ilianzisha kikosi cha IFOR, ambacho kilifuatiwa na Kikosi cha Udhibiti cha SFOR, kudumisha usitishaji wa mapigano na kuleta utulivu katika taifa hilo dogo la kusini mashariki mwa Ulaya.

Soma pia:Viongozi wa NATO kujadili msaada zaidi kwa Ukraine

Ujerumani ilishiriki, lakini jeshi lake, Bundeswehr lilitayarishwa kwa sehemu tu kwa ujumbe katika nchi hiyo ya milimani. Wanajeshi wa Ujerumani hawakuwa wamepatiwa mafunzo kwa ajili ya operesheni za "nje ya eneo".

Wakati wa Vita Baridi, jeshi la Shirikisho la Ujerumani Magharibi, ambalo lilijiunga na NATO mwaka 1995, lilikuwa na jukumu la kujilinda dhidi ya uwezekano wa shambulizi linalowezekana la nchi zilizosaini Mkataba wa Warsaw, ambazo zilikuwa katika eneo la ushawishi wa Kisovieti na ziliijumuisha Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani Mashariki, GDR.

Kulikuwa na nusu milioni ya askari wa Kisovieti waliopelekwa Ujerumani Mashariki. Na Jeshi la Taifa la Wananchi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani, NVA, lilijivunia zaidi ya askari 150,000 wa ziada.

Kuanzia mwaka 1958 hadi 1972, jeshi la Ujerumani Magharibi liliongezeka kutoka askari 249,000 hadi 493,000. Hadi kuanguka kwa Ukuta wa Berlin, idadi ya wanajeshi ilikuwa takribani 480,000.

Wakati Bundeswehr ilipounganishwa na Jeshi la Taifa la Wananchi, kwa lengo kuu la kumaliza mundo wake, idadi iliongezeka tena kwa muda mfupi.

Mafunzo kwa wanajeshi wa Bundeswehr

Takribani miaka 20 badaae, kulikuwa na kiasi cha wanajeshi 200,000 tu waliobakia katika Bundeswehr. Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani, kufikia mwaka 2023, kulikuwa na wanajeshi 181,000 pekee.

NATO ni nini?

02:15

This browser does not support the video element.

Ni sehemu ndogo tu ya wanajeshi hawa waliopata mafunzo na kupelekwa kwa ajili ya mapambano kama sehemu ya ujumbe wa NATO.

Jukumu la Jeshi la Ujerumani ndani ya NATO lilibadilika tena baada ya mashambulizi yaliyotokea nchini Marekani Septemba 11, mwaka 2001, yaliyosababisha Marekani kutumia kipengele cha ulinzi wa pamoja cha NATO, na Ujerumani ilitimiza wajibu wake wa mkataba.

Soma pia:Uholanzi yatangaza kuisaidia Ukraine mfumo wa kujilinda angani

Jeshi la Ujerumani lilikuwa sehemu ya jeshi la muungano lililoongozwa na Marekani ambalo liliivamia Afghanistan kwa lengo la kuwarudisha nyuma wanamgambo wa Taliban.

Wakati wa Vita Baridi na tangu miaka hiyo, Marekani imekuwa na jukumu kubwa ndani ya NATO. Lakini ulinzi wa Marekani unaweza kupotea iwapo Donald Trump atachaguliwa tena kuwa rais wa Marekani.

Trump ametishia kutowalinda washirika wa NATO ambao hawatumii pesa za kutosha kwa ajili ya kujilinda na Uru

Scholz: Bundeswehr lazima inadhamana ya ulinzi NATO

Waziri wa Ulinzi Ujerumani Boris Pistorius akiwa na wanajeshi Picha: Christoph Hardt/Panama Pictures/picture alliance

Je Ujerumani, itachukua jukumu kubwa ndani ya NATO katika siku zijazo? Akitoa taarifa ya serikali Juni 2023, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, alisema Bundeswehr lazima iwe mdhamini wa ulinzi wa kawaida barani Ulaya, ingawa bado haina wafanyakazi, vifaa na uwezo wa kufanya hivyo.

Tangu wakati huo, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius alisema kwamba jeshi la nchi hiyo linapaswa "kujiandaa kwa vita." Baadhi ya wachambuzi wanahisi kuwa Urusi inaweza kuanzisha mashambulizi kwenye eneo la NATO katika muda wa chini ya miaka mitano.

Kwa hivyo, wazo sasa ni kuiboresha NATO kwa kiwango ambacho inaweza kuwa kizuizi kikubwa kwa Urusi kushambulia eneo la NATO. Kama ilivyokuwa katika miongo minne ya Vita Baridi.