1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Ujerumani Mashariki ya Kati ?

26 Julai 2006

Uchambuzi wa wahariri leo umetuwama juu ya athari za kutumika kwa Jeshi la Ujerumani Mashariki ya kati, lakini pia madereva wanagenzi mwiko kunywa pombe:

Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG laandika kuwa hoja kali ya kuvishirikisha vikosi vya Ujerumani katika kusimamia amani huko mashariki ya kati bila ya shaka yoyote ni kuwapo kwa dola la Israel na hilo ni jukumu Ujerumani kulibeba.

Lakini hii maana yake kutetea kuwapo kwa dola la Israel wajerumani wanabidi hata kushika bunduki ?

Wazi ni kuwa, dai kuwa vikosi vitakavyowekwa kulinda amani viwe imara , maana yake pia kuwa tayari kuwafyatulia risasi wapiganaji wa Hizbollah.Mbaya zaidi ni kuuliza:kitatokea nini endapo vikosi hivyo vya kuhifadhi amani vikibidi kukizuwia kikundi cha makando cha Israel kuwaandama wanamgambo wa Hizbollah ?

Ama gazeti linalo chapishwa mjini Frankfurt Order-MÄRKISCHE ODERZEITUNG laandika kuwea yamkini Israel inapendelea kuwekwa kwa vikosi vya kimataifa kusini mwa Lebanon.Serikali ya Lebanon lakini ,ingependelea kulitatua tatizo la Hiozbollah kisiasa na sio kwa mtutu wa bunduki.

Uamuzi wa haraka wa waziri wa ulinzi wa Ujerumani unabainisha wazi siasa inayoongoza mara kwa mara katika msukosuko. Kwamba, kanzela Angela Merkel anakwepa kukaripia ,haitoi heba nzuri kwake.

Gazeti la MÄRKISCHE ALLGEMEINE kutoka Potsdam lina hakika kwamba ikija kuliangukia jeshi la Ujerumani-Bundeswehr kuyazuwia majeshi ya Israel yasishambulie nchini Lebanon,basi Ujerumani isishiriki katika kuhifadhi amani.Kwani baada ya mkasa wa Holocaust-wa kuwahilikisha wayahudi ,ni vigumu kufikiria tena kwa wanajeshi wa Ujerumani kuwafyatulia tena risasi wayahudi.Ikiwa tangu Israel hata Syria zitaridhia kuwapo kwa wanajeshi wa Ujerumani, huko Mashariki ya kati,basi serikali ya Ujerumani haiwezi kuwakatalia ombi hilo- MÄRKISCHE ALLGEMEINE.

Likitubadilishia mada,madereva waliopata punde hivi leseni zao za kuendesha magari pengine kuanzia mwakani watapaswa wasinywe pombe kabisa.Kwa muujibu wa wizara ya usafiri,baraza la mawaziri linapanga baada ya likizo hii ya majira ya kiangazi kuzingatia sheria hiyo.Sheria hiyo inapanga kuzuwia kabisa kuendfesha gari ikiwa mtu amekunywa pombe.wahariri wa magazeti ya Ujerumani wameijadili sheria hii:

Gazeti la MORGENPOST linalotoka Berlin lasema :

“Kumpiga marufuku kunywa pombe dereva mwanagenzi kama inavyopanga serikali ya ujerumani ni hatua muhimu kuimarisha usalama barabarani na kupunguza zaidi idadi ya ajali majiani.Hatari ya pombe iko katika kujiamini kupita kiasi kwa dereva mchanga kwamba angeweza kudhibiti usukani.Dai la kumpiga marufuku dereva mwana-genzi kunywa pombe japo kidogo na kuendesha gari ni barabara kiusalama.Kisiasa lakini, kuipitisha sheria hiyo,lasema gazeti, haitawezekana.