1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Jeshi la Ukraine ladungua droni tano za Urusi

16 Agosti 2024

Jeshi la anga la Ukraine limesema leo kuwa limefanikiwa kuzidungua droni tano za Urusi wakati wa shambulio lililofanyika usiku wa kuamkia leo.

Hochhaus in russischer Stadt Belgorod bei Angriff getroffen
Picha: Russian Defence Ministry/AFP

Kulingana na taarifa ya jeshi la Ukraine kupitia mtandao wa Telegram, vikosi vya Urusi vilitumia makombora matatu ya balestiki aina ya Iskander-M na droni tatu aina ya Shahed na aina isiyojulikana ya droni nyengine mbili wakati wa shambulio hilo.

Magavana wa mikoa ya Kyiv na Kirovohrad wameeleza kuwa shambulio hilo la Urusi halikusababisha uharibifu wala majeraha yoyote.

Shirika la habari la Reuters limewahi kuripoti kwamba Urusi imegeukia matumizi ya droni zilizotengezwwa kwa bei nafuu katika baadhi ya mashambulizi yake ili kupima uimara wa mfumo wa anga wa Ukraine.