1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Jeshi la Ukraine lashambulia ghala la mafuta ndani ya Urusi

8 Januari 2025

Jeshi la Ukraine limesema leo Jumatano kwamba limeshambulia ghala la kuhifadhi mafuta ndani ya Urusi, na kusababisha moto mkubwa kwenye kituo hicho ambacho hutoa huduma muhimu kwa kikosi cha anga cha Urusi.

Vita vya Ukraine
Vita vya UkrainePicha: Russian Defense Ministry/AP/picture alliance

Jeshi la Ukraine limesema leo Jumatano kwamba limeshambulia ghala la kuhifadhi mafuta ndani ya Urusi, na kusababisha moto mkubwa kwenye kituo hicho ambacho hutoa huduma muhimu kwa kikosi cha anga cha Urusi.

Maafisa wa Urusi wamekiri kutokea kwa shambulio hilo kubwa la dronikatika eneo hilo na kusema kwamba mamlaka yake imechukua hatua za haraka kwa kuanzisha kituo cha dharura ili kusaidia kupambana na athari zilizosababishwa na shambulio hilo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema mwaka jana kuwa nchi yake imetengeneza silaha za masafa marefu zenye uwezo wa kushambulia umbali wa kilomita 700 na droni zenye uwezo wa kusshambulia zaidi ya kilomita 1000. Zelensky alisema lengo lao ni kuyashambulia maeneo ya ndani zaidi ya Urusi.

Nchi zote mbili Urusi na Ukraine bado zinaendelea kushambuliana katika mzozo ambao umedumu kwa karibu miaka mitatu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW