MigogoroUkraine
Jeshi la Ukraine limedungua droni 21 za Urusi
9 Oktoba 2024Matangazo
Jeshi hilo limesema limedungua droni 21, na nyingine ilirejea kuelekea upande wa Urusi. Wakati huo huo, Gavana wa Jimbo la Odesa, Oleh Kiper, amesema droni la Urusi kwenye jimbo hilo limewajeruhi watu watano na kuharibu jengo la ghorofa.
Aidha, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema mitambo yake ya kujikinga na makombora, imeharibu droni 47 za Ukraine zilizorushwa kwenye eneo lake la magharibi. Maafisa wamesema mashambulizi hayo hayajasababisha madhara yoyote.
Wizara hiyo imesema takriban droni 24 zilidunguliwa kwenye eneo la mpaka wa kusini magharibi wa jimbo la Bryansk, na nyingine ziliharibiwa katika majimbo ya Belgorod, Kursk, Rostov na Krasnodar, na kwenye eneo la Bahari ya Azov.