1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi Guinea-Bissau limewaachia viongozi waliokuwa kizuizini

1 Desemba 2023

Waziri wa Fedha Souleiman Seidi na Katibu Antonio Monteiro waliokuwa wametiwa kizuizini na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi kufuatia tukio la ufyatulianaji risasi na vikosi maalum wameachiliwa huru na jeshi la ulinzi.

Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embaló ahutubia kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Alhamisi, Septemba 21, 2023
Rais wa Guinea Bissau Umaro Sissoco EmbalóPicha: Craig Ruttle/AP Photo/picture alliance

Vyanzo vyajeshi walivyozungumza kwa masharti ya kutokutajwa majina, ''polisi waliwahoji maafisa hao wawili kwa saa kadhaa kuhusu kupotea kwa dola milioni 10 kutoka kwa hazina ya serikali.

Katika kikao cha bunge siku ya Jumatatu, wabunge walimuhoji Seidi juu ya kujiondoa katika kikao chaBunge la Kitaifa, ambapo alijitetea kwa kusema, kujiondoaa kwake kulikuwa kisheria na kwa maslahi ya taifa.

Soma zaidi: Umeme warejeshwa Bissau baada ya serikali kulipa deni

Vyanzo hivyo vimesema, maafisa wa ulinzi wa kitaifa waliwachukua Seidi na Monteiro hadi eneo lisilojulikana Alhamisi usiku kabla ya kukimbilia katika kambi iliyopo kusini mwa wilaya ya Santa Luzia.

Mwandishi wa Shirika la habari la Ufaransa amesema, milio ya risasi ilisikika karibu na kambi ya kitongoji hicho, huku vikosi maalum vikiingilia kati baada ya majaribio kadhaa ya upatanishi kufanyika bila kuwepo mafanikio. 

Gwaride la jeshi likipita katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Guinea-BissauPicha: Iancuba Danso/DW

Pia ameeleza kuwa, Wanachama wa Kikosi cha Kusaidia Utulivu cha Guinea-Bissau, kilichotumwa nchini humo na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), walionekana wakishika doria katika mitaa ya mji mkuu Bissau. 

Waandishi wa Reuters wamesema, milio hiyo ya risasi ilisikika usiku kucha katika mji mkuu wa Guinea-Bissau na kuendelea hadi Ijumaa asubuhi kitongoji cha Antula, ambapo jenerali wa jeshi anaishi, huku magari ya kijeshi yakiwa yameenea mitaani.

Huu ni mfuulizo wa tukio la 10 la jaribio la mapinduzi nchini Guinea Bissau tangu nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka 1974. Huku takribani watu sita wakipoteza maisha katika jaribio la kumpindua Rais Umaro SissocoEmbalo Februari mwaka jana.

Soma Zaidi: Viongozi wa Afrika Magharibi waitisha mkutano wa dharura baada ya mapinduzi

Japo Rais Umaro Sissoco Embaló alisema mapambano hayo ni vita dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya na si mpango wa jeshi wa kutaka kuchukua madaraka. Wakati hayo yakijiri Rais Embaló, aliyeingia madarakani Disemba 2019, yupo Dubai kuhudhuria Mkutano wa 28 wa Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa (COP28).

Embaló aliwateua majenerali wawili Tomas Djassi kuwa Mkuu wa Usalama wa Rais na Horta Inta, kuwa Mkuu wa Majeshi ili kuimarisha usalama wake. Kuimarishwa huku kwa usalama wa rais kunakuja wakati majaribio ya mapinduzi yanaongezeka ukanda wa Afrika Magharibi, hasa nchi za Gabon, Niger, Mali, Burkina Faso, Guinea na, Sierra Leone.

ECOWAS wametoa tamko juu mizozo inayondelea nchi za Afrika Magharibi

Viongozi wa Afrika Magharibi watafanya mkutano wa kilele mwishoni mwa mwezi huu wakati eneo hilo likijitahidi kubadili mfululizo wa mapinduzi na kuzuia mizozo ya wanajihadi katika Sahel.

Viongozi hao ambao walikutana mara ya mwisho mwezi Agosti kwa mazungumzo kuhusu Niger baada ya mapinduzi ya Julai 26 huko ambayo yalimpindua rais mteule Mohamed Bazoum.

Mwanyekiti wa ECOWAS ambae pia ni Rais wa Nigeria Bola TinubuPicha: Gbemiga Olamikan/AP/dpa/picture alliance

Wakuu wa nchi za ECOWAS walitishia kuingilia kijeshi kama njia ya mwisho ya kumrejesha Bazoum na kuiwekea Niger vikwazo vizito vya kiuchumi, ambayo sasa inatawaliwa na utawala wa kijeshi unaoongozwa na Jenerali Abdourahamane Tiani.

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu, ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS, anasema mazungumzo ya pande mbili bado yanaendelea na serikali ya Niger.

Kamishna wa ECOWAS wa masuala ya kisiasa, Abdel-Fatau Musah katika mahojiano yake Alhamisi alisema  "Mambo mengi yanaweza kujadiliwa, lakini kwa hali yoyote hawatakubali mpito wa miaka mitatu wala umoja huo hauwezi kutambua serikali ya kijeshi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW