1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Jeshi la Urusi ladai kuteka kijiji kingine cha Ukraine

25 Agosti 2025

Jeshi la Urusi limedai kukikamata kijiji kingine kwenye jimbo la Dnipropetrovsk na kuzidi kuingia kwenye maeneo ya Ukraine, huku hatua za kupatikana kwa makubaliano ya amani kwa mara nyingine zikikwama.

Ukraine | Dnipropetrovsk
Kikosi cha uokozi kikiwa kimembeba mwanamke aliyejeruhiwa baada ya shambulizi la Urusi lililoangusha jengo kwenye jimbo la Dnipropetrovsk, Ukraine, Juni 24, 2025Picha: State Emergency Service of Ukraine in Dnipropetrovsk region/REUTERS

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imeesema vikosi vyake vimeteka eneo la Zaporizke, ambako hivi karibuni wanajeshi wa Urusi waliingia kwa mara ya kwanza tangu vita vilipozuka miaka mitatu na nusu iliyopita.

Urusi imeanzisha mashambulizi ya droni ya usiku kucha nchini Ukraine, ikilenga mkoa wa mpakani wa Sumy na kumuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine tisa, hii ikiwa ni kulingana na Gavana Oleh Hryhorov mapema leo, kupitia mtandao wa Telegram.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW