1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Jeshi la Urusi ladai kuuteka mji mmoja mashariki mwa Ukraine

8 Septemba 2024

Jeshi la Urusi limesema leo kuwa limeteka mji wa Novohrodivka mashariki mwa Ukraine, ambapo vikosi vyake vinasonga mbele kuelekea mji wa kimkakati wa Pokrovsk.

Wanajeshi wa Ukraine wapumzika wakati wa mazoezi katika eneo la Sumy karibu na mpaka wa Urusi mnamo Agosti 17,2024, huku vita vikiendelea katika ya nchi hizo mbili.
Wanajeshi wa Ukraine wapumzika wakati wa mazoezi katika eneo la Sumy karibu na mpaka wa UrusiPicha: Thomas Peter/REUTERS

Katika taarifa, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema kuwa vikosi vya nchi hiyo vimeuteka mji huo wa Novohrodivka katika eneo la Donetsk, umbali wa kilomita 20 kutoka mji wa Pokrovsk.

Mji huo ulikuwa na zaidi ya wakazi 14,000 kabla ya kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari mwaka 2022, hii ikiwa ni kulingana na takwimu rasmi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amteuwa mshauri wa nje wa masuala ya kimkakati

 Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, leo amemteuwa aliyekuwa waziri wa viwanda vya silaha, Oleksandr Kamyshin, kama mshauri wa nje wa masuala ya kimkakati. Haya ni kwa mujibu wa amri iliyochapishwa kwenye tovuti ya urais.

Kamyshin, alijiuzulu kama waziri wiki iliyopita kama sehemu ya mabadiliko kwenye serikali ya Ukraine katika wakati mgumu wa vita vyake na Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW