1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Urusi lasema Ukraine imefyatua kombora la masafa

19 Novemba 2024

Jeshi la Urusi limesema, Ukraine imefyetuwa makombora kadhaa ya masafa marefu iliyopewa na Marekani, iliyolenga kituo kimoja cha kijeshi katika eneo la mpakani la Bryansk.

US-Armee | taktische Raketensystems (ATACMS)
Rais wa Marekani Joe Biden ametoa ridhaa kwa Ukraine kutumia makombora ya masafa marefu yaliyotolewa na Marekani kuishambulia Urusi.Picha: U.S. Army/ABACA/picture alliance

Shambulio hilo la Ukraine ni la kwanza linalohusisha silaha za  Marekani,tangu rais Joe Biden alipoiruhusu Kiev kutumia makombora yake ya masafa marefu dhidi ya Urusi. Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema makombora sita ya masafa marefu aina ya ATACM yamefyetuliwa na Ukraine alfajiri ya leo Jumanne lakini ikaongeza kwamba hakuna vifo wala uharibifu ulioripotiwa. Moscow ilishaonya kwamba kutumiwa silaha za mataifa ya Magharibi kuishambulia, ni hatua itakayoifanya Marekani kuwa muhusika wa moja kwa moja katika vita hivyo na itachukuliwa hatua kali.