Jeshi la Uturuki lawahujumu PKK kaskazini mwa Irak
16 Desemba 2007Matangazo
Ankara:
Jeshi la wanaanga la Uturuki limehujumu vituo vya waasi wa chama cha wafanyakazi wa kikurd-PKK,kaskazini mwa Irak.Madege manane ya kijeshi ya Uturuki yameshiriki katika hujuma hizo karibu na mlima Kandil-kaskazini mwa Irak.Majumba mawili ya waasi yamehujumiwa na mkuu mmoja wa waasi anasemekana pia kauliwa.Waasi wa PKK hawajadhibitisha lakini habari hizo.Eneo hilo la milimani linaangaliwa kama ngome ya waasi wa kikurd wa PKK wanaofanya mashambulio dhidi ya wanajeshi wa uturuki nchini Uturuki.Marekani inawapatia maelezo wanajeshi wa Uturuki kuhusu wapo vinakutikana vituo vya waasi wa PKK kaskazini mwa Irak.