1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Iran yazikamata meli mbili kwenye Mlango Bahari wa Hormuz

22 Aprili 2026

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi la Iran imezikamata meli mbili katika Mlango Bahari wa Hormuz Jumatano, hali inayoongeza mvutano kati ya Tehran na Marekani kuhusu njia hiyo muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani.

Iran imezikamata meli mbili kwenye Mlango Bahari wa Hormuz
Mlango Bahari wa HormuzPicha: Dado Ruvic/REUTERS

Kulingana na shirika la habari la Tasnim, jeshi la Walinzi wa Mapinduzi limezikamata meli hizo kutokana na kukiuka sheria za baharini na lilizisindikiza hadi kwenye fukwe za Iran.

Ni meli za kwanza kukamatwa tangu kuanza kwa vita

Hii ni mara ya kwanza Iran kukamata meli katika eneo hilo tangu vita vilipoanza mwishoni mwa mwezi Februari. Awali, jeshi la Iran liliripoti kuzishambulia meli tatu za  makontena kwenye Mlango Bahari wa Hormuz ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Haya yanajiri wakati ambapo Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kusitisha mashambulizi dhidi ya Tehran kwa muda usiojulikana, kufuatia ombi kutoka kwa wapatanishi wa Pakistan ili kupisha mazungumzo ya usuluhishi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW