1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhamiajiSenegal

Jeshi la wanamaji la Senegal laopoa miili 30

23 Septemba 2024

Jeshi la wanamaji la Senegal limeiopoa takriban miili 30 kutoka kwenye boti iliyopatikana usiku wa kuamkia leo karibu kilomita 70 kutoka pwani ya mji mkuu Dakar.

Bassirou Diomaye Faye | Rais wa Senegal
Rais wa Senegal Diomaye Faye akiahidi kukabiliana na magenge ya wahalifu yanayowasafirisha watu kimagendoPicha: Dylan Martinez/AFP

Mamlaka za jeshi hilo zimeeleza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini sehemu ilikotoka meli hiyo na kuthibitisha idadi ya waliofariki.

Ukanda wa pwani wa Senegal unashuhudia vifo vya mara kwa mara vinavyohusisha majaribio ya wahamiaji kutaka kuingia Ulaya kwa kutumia mashua.

Mwezi Septemba, takriban watu 39 walifariki baada ya mashua yao kuzama karibu na mji wa bandari wa Mbour, magharibi mwa nchi hiyo.

Wakati rais wa Senegal Diomaye Faye akiahidi kukabiliana na magenge ya wahalifu yanayowasafirisha watu kimagendo, tangu kuanza kwa mwaka huu, wahamiaji 22,000 wamewasili kwenye visiwa vya Canary nchini Uhispania.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW