1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSenegal

Jeshi la wanamaji la Senegal lawakamata wahamiaji 200

27 Julai 2024

Jeshi la wanamaji la Senegal limekamata siku ya Ijumaa mashua iliyokuwa imewabeba wahamiaji 200 katika mji wa bandari wa kaskazini wa Saint Louis.

Senegal | Ajali ya boti ya wahamiaji wanaojaribu kuingia UIaya.
Raia wa Senegal wakijaribu kuivuta boti baada ya ajali iliyosababisha vifo vya watu kadhaa: 24.07.2024Picha: Leo Correa/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa jeshi amesema watu hao kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wamepelekwa mjini Dakar kwa ukaguzi zaidi.

Tukio hili linajiri siku chache baada ya watu 90 kufa maji kwenye pwani ya Mauritania walipokuwa wakijaribu kuvuka eneo hilo ili kuelekea barani Ulaya. Siku ya Jumatatu, takriban watu 25 walikufa katika  ajali ya meli  karibu na mji mkuu wa Mauritania Nouakchott.

Waziri Mkuu wa Senegal, Ousmane Sonko amewataka watu kutohatarisha maisha yao kwenye Bahari ya Atlantiki kwa kujaribu kuingia Ulaya. Lakini njia hiyo inazidi kutumiwa huku mamlaka zikiongeza ufuatiliaji katika Bahari ya Mediterania.

Soma pia: Wahamiaji 61 wapoteza maisha baharini njiani kwenda Ulaya

Kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Uhispania la "Caminando Fronteras", katika kipindi cha miezi mitano ya mwanzo ya mwaka huu, zaidi ya watu 5,000 wamekufa wakijaribu kuwasili katika Visiwa vya Canary vya Uhispania.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW