1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGabon

Jeshi lamtangaza Brice Nguema kama kiongozi wa mpito Gabon

31 Agosti 2023

Viongozi wa kijeshi waliochukua madaraka nchini Gabon wamemtangaza mkuu wa kitengo cha walinzi wa rais, Brice Clotaire Oligui Nguema, kama kiongozi wa mpito.

Viongozi wa kijeshi wa Gabon wakitangaza kutwaa madaraka Gabon baada ya kuchaguliwa tena kwa Rais Ali Bongo
Viongozi wa kijeshi wa Gabon wakitangaza kutwaa madaraka Gabon baada ya kuchaguliwa tena kwa Rais Ali BongoPicha: Gabon 1ere/REUTERS

Brice Nguema, kulingana na ripoti za vyombo vya habari ni binamu wa rais aliyeondolewa madarakani Ali Bongo.

Msemaji wa linalojulikana kama baraza la mpito, kupitia shirika la habari la serikali la Gabon 24, alimtangaza Nguema kama rais wa mpito jana jioni.

Saa chache baada ya viongozi wa kijeshi kutwaa mamlaka, Rais Ali Bongo alionekana kwenye ukanda wa video akitoa wito wa usaidizi kutoka sehemu alikozuiliwa.

Bongo amewataka raia wa Gabon "kupiga kelele" na kueleza kuwa amezuiliwa kinyume cha sheria katika maakazi yake.

Kundi la maafisa wa ngazi ya juu jeshini wameiambia televisheni ya taifa kuwa Bongo anatuhumiwa kwa uhaini mkubwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW