1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi na polisi Venezuela wasimama kidete na rais Maduro

Sylvia Mwehozi
7 Agosti 2024

Jeshi na vikosi vya polisi wa Venezuela hapo jana vilithibitisha utiifu wake kwa rais Nicolas Maduro, wakati tume ya uchaguzi ikisema kuwa imewasilisha matokeo rasmi ya uchaguzi kwa mahakama kuu.

Venezuela -Nicolas Maduro
Rais wa Venezuela Nicolas MaduroPicha: Presidency of Venezuela/Xinhua/picture alliance

Jeshi na vikosi vya polisi wa Venezuela hapo jana vilithibitisha utiifu wake kwa rais Nicolas Maduro, wakati tume ya uchaguzi ikisema kuwa imewasilisha matokeo rasmi ya uchaguzi kwa mahakama kuu.Shinikizo kwa Nicolas Maduro lazidi kuongezeka

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na wizara ya ulinzi na ile ya mambo ya ndani, ilisema kuwa vikosi vya usalama vya nchi hiyo vinasimama kidete na rais Maduro.

Taarifa hiyo inafuatia barua ya wazi iliyowasilishwa na kiongozi wa upinzani Maria Corina Machado na mgombea wa urais wa upinzani Edmundo Gonzalez, iliyowatolea wito wanajeshi na polisi kuungana na wananchi na kuacha kufuata maelekezo ya Maduro.

Wito wao ulijibiwa na tangazo la kuanzishwa haraka uchunguzi wa kihalifudhidi ya viongozi hao wa upinzani.