1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jill Biden kushuhudia kutawazwa kwa Mfalme Charles III

6 Mei 2023

Mke wa rais Joe Biden wa Marekani, Jill ni miongoni mwa wageni maarufu watakaohudhuria sherehe za kutawazwa kwa Mfalme Charles III wa Uingereza zinazofanyika hii leo

USA Jill Biden  bei der Benefizgala des Costume Institute des Metropolitan Museum of Art 2022
Picha: Charles Sykes/dpa/Invision/picture alliance

Shughuli za uapisho zitafanyika Westminster Abbey na kuhudhuriwa na mamia ya viongozi wa mataifa mbalimbali na wageni walioalikwa kushuhudia Mfalme Charles na mkewe Camilla wakitawazwa kuwa mfalme na malkia.

Soma zaidi:Charles III atangazwa rasmi kuwa Mfalme wa Uingereza

Akiwa London, Jill atakutana na mke wa waziri mkuu Rishi Sunak, Akshata Murty katika makazi yao yaliyopo mtaa wa Downing na kutembelea ubalozi wa Marekani nchini humo na baadae kuhudhuria hafla iliyoandaliwa na mfalme katika kasri ya Buckingham.

Ingawa hakuna rais wa Marekani aliyewahi kuhudhuria shughuli hiyo, lakini hatua ya Biden ya kushindwa kuhudhuriwa imekosolewa pakubwa. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW