Jimbo la Wakurd lashutumu mashambulizi ya Uturuki.
18 Desemba 2007Matangazo
Sulaimania , Iraq.
Serikali ya jimbo lenye madaraka yake ya ndani la Wakurd nchini Iraq leo imeshutumu mashambulizi ndani ya mpaka wa nchi hiyo yaliyofanywa na majeshi ya Uturuki .
Fouad Hussein , mkuu wa ofisi ya rais wa jimbo hilo la Wakurd Mahmoud barzani , amesema kuwa Uturuki inataka kuhamishia matatizo yake katika jimbo hilo la Iraq. Ameongeza kuwa hafahamu ukumbwa wa jeshi la Uturuki ambalo limevuka mpaka na kuingia nchini Iraq.