1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jimbo lenye utajiri wa madini DRC lasimamisha uchimbaji

20 Julai 2024

Mamlaka katika moja ya jimbo moja lenye utajiri mkubwa wa madini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imetangaza kusimamishwa kwa shughuli zote za uchimbaji madini ili "kurejesha utaratibu" katika sekta hiyo.

DR Congo | Mgodi wa dhahabu wa Luhihi katika mkoa wa Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Mchimbaji akisafisha dhahabu kwenye maabara ya Primera Gold huko Bukavu, Mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mei 12, 2023.Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Afisa Habari wa jimbo hilo la Kivu ya Kusini Danny Bashige, amesema Gavana wa jimbo hilo Jean-Jacques Purusi "anataka kudhibiti uchimbaji holela ya madini katika eneo hilo." Pasipo kutoa ufafanuziwa kina taarifa ya Gavama huyo inasema "shughuli za uchimbaji madini zimesitishwa hadi itakapotangazwa tena kwa sababu ya "usumbufu unaosababishwa na waendeshaji madini.”

Pamoja na sababu hiyo nyingne sio tu kuyalinda maisha ya watu, lakini pia ufuatiliaji wa uzalishaji wa madini katika maeneo hayo. Kutokana na taarifa hiyo makampuni ya uchimbaji madini, wafanyabiashara na washirika wengine wamepewa masaa 72 kuondoka katika maene ya machimbo.

Tathmini ya athari za kiuchumi kwa wakazi katika maeneo ya madini

Wachimbaji dhahabu wakisimama katika mgodi wa dhahabu wa Luhihi katika jimbo la Kivu ya Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mei 13, 2023.Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Lakini hata hivyo limekuwa jambo gumu kutoa tathimini athari ya agizo hilo mara moja. Maelfu ya wakazi

wa jimbo hilo lenye utajiri wa madini ya dhahabu na koltan hutegemea moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwenye uchimbaji madini. Hapo awali mamlaka zimewahi kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo hilo, lakini kumekuwa na matokeo madogo.

Kivu ya Kusini ina madini mengi yakiwemo dhahabu, cassiterite na koltan ambayo yanachimbwa na makampuni ya kigeni, hasa ya China.

Hatari ya kila mara katika maeneo ya uchimbaji madini

Uchimbaji madini katika eneo hilo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa muda mrefu umekuwa katika makabiliano ya ghasia kutoka kwa makundi yenye kujihami kwa silaha na usafirishaji wa madini kwenda nchi jirani, kama vile Rwanda.

Mashambulizi kwenye machimbo na vyama vya ushirika vya uchimbaji madini yanatokea mara kwa mara katika eneo hilo ambalo lina makundi zaidi ya 120 yenye kujihami kwa silaha yakishindania ardhi na rasilimali mashariki mwa Kongo.

Soma zaidi:Makubaliano yasitisha mapigano nchini DRC yarefushwa kwa siku 15 zaidi

Mapema mwezi huu, wanamgambo walishambulia mgodi wa dhahabu katika mkoa wa Ituri kaskazini mashariki mwa Kongo ambapo waliwaua wachimba migodi sita wa Kichina na wanajeshi wawili wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Chanzo: AFP