1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Jimbo lililojitenga la Somaliland lafanya uchaguzi wa rais

13 Novemba 2024

Somaliland, jimbo lililojitenga na Somalia, linafanya uchaguzi wa rais siku ya Jumatano.

Somaliland | Uchaguzi wa rais
Rais wa sasa wa jimbo la Somaliland Muse Bihi anakabiliana na Abdirahman Mohamed Abdullahi wa chama cha Waddani.Picha: TIKSA NEGERI/REUTERS

Rais wa Somaliland Muse Bihi, anakabiliana na mpinzani wake mkubwa Abdirahman Mohamed Abdullahi wa chama cha Waddani.

Mohamed Abdullahi, mwanadiplomasia wa zamani na Spika wa muda mrefu wa Bunge la Somaliland katika mchuano huo anatetea sera chache za mabadiliko, na amesisitiza kwamba atakuwa kielelezo cha muungano.

Wakosoaji, wanamshutumu Bihi kwa utawala wa kiimla uliochochea mgawanyiko miongoni mwa makabila.

Uchaguzi huu unafanyika wakati eneo hilo likimulikwa kimataifa kufuatia mzozo mkubwa kati ya Somalia na Ethiopia, baada ya makubaliano ya ukodishaji wa bandari baina ya Addis Ababa na Somaliland, ambayo Somalia inayapinga.

Hata hivyo wagombea wote wanaunga mkono hatua hiyo iliyochukuliwa na rais wa sasa Muse Bihi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW