1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fahamu wajumbe maalum Marekani wanavyochagua rais

6 Novemba 2024

Rais mpya wa Marekani, huwa hachaguliwi moja kwa moja na kura za wananchi walio wengi kama ilivyo kwenye demokrasia ya kawaida, bali kupitia kile kiitwacho kura za wajumbe wa kamati maalum ya uchaguzi.

Uchaguzi wa Marekani
Uchaguzi wa MarekaniPicha: DW

Mfumo wa kura za wajumbe wa kamati maalum ya uchaguzi ulianzishwa na waasisi wa Katiba ya Marekani mwaka 1787, wakati huo Marekani likiwa ndio kwanza ni taifa jipya huru kufuatia kujikombowa kutoka ukoloni wa Uingereza kupitia vita. 

Waasisi wa taifa hilo walitaka kuanzisha mfumo wa uchaguzi ambao hautakusanya madaraka yote mahala pamoja, wakiazimia kukwepa muundo wa utawala wa kifalme kama ule ambao walikuwa ndio kwanza wamejikomboa.Uchaguzi wa Marekani: Nini kinatokea siku ya uchaguzi na baadae?

Hata hivyo, wazo la uchaguzi unaowahusisha watu wote waliuona una changamoto zake, mojawapo ni kwamba waliwaona wapigakura watarajiwa wakiwa hawana elimu ya kutosha kuweza kufanya maamuzi sahihi kupitia kura zao.

Wakati huo, idadi ya wasiojuwa kusoma na kuandika ilikuwa chini, na wakati huo hakukuwa na nchi ambayo ilikuwa ikichaguwa viongozi wake kupitia kura ya wengi.

Kwa hivyo, waasisi wa katiba wakaona Kura za Wajumbe kuwa muafaka baina ya kura ya wengi na kukipa chombo kimoja dhamana ya kumchaguwa rais. Ndipo walipoamua kuwachaguwa wachaguwaji kwenye kila jimbo ili nao wamchaguwe rais.

Mfumo wa Kura za Wajumbe unavyofanya kazi

Serikali ya Marekani inaundwa kinadharia na baraza la mawaziri linalomjumuisha rais na mawaziri wake, mahakama kwa maana ya Mahakama ya Juu na bunge, ambalo linaundwa kwa mabaraza mawili: la Wawakilishi na Seneti. Kila jimbo lina wajumbe wawili kwenye Baraza la Seneti.Uchaguzi Marekani: Washington yasalia tulivu kabla ya kivumbi

Harris kuchuana vikali na Trump. Nani kuibuka mshindi leo?

03:04

This browser does not support the video element.

Hawa wanawakilisha jimbo kwenye kiwango cha shirikisho. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanawakilisha wilaya ndani ya majimbo hayo. Idadi ya wawakilishi wa bunge kwa kila jimbo inaamuliwa na sensa ya watu ambayo hufanyika kila baada ya miaka kumi.

Carlifornia ndilo jimbo lenye idadi kubwa zaidi ya watu, na hivyo lina wajumbe wengi zaidi: 52 jumla yao.

Majimbo yenye idadi ndogo zaidi ya watu, kama vile Alaska, yanakuwa na mjumbe mmoja tu. Kila jumbe huwa lina kura moja kwa kila mjumbe mmoja bungeni.

Hiyo maana yake  ni kuwa jimbo la California lina kura 54 za wajumbe, yaani 52 kutoka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na mbili kwa wajumbe wake wa Baraza la Seneti. Alaska ina kura tatu: moja kwa Baraza la Wawakilishi na mbili kwa maseneta wake.Harris, Trump wafanya kampeini za mwisho Pennsylvania

Kwa ujumla, kuna wajumbe 535 wa Bunge, au kama waitavyo wenyewe, Congress, kwa kuwa kuna wajumbe watatu kwenye makao makuu ya nchi, Washington D.C, inamaanisha kuna kura 538 za wajumbe ambazo zinawaniwa na wanaogombea urais. Ili mgombea atangazwe mshindi, anahitaji kupata kura 270 kati ya hizo.

Wamarekani wanamchagua nani?

Jibu ni kwamba, wakati raia wa Marekani wanapopiga kura kwenye uchaguzi wa rais, huwa wanawapigia kura wachaguwaji wa mgombea wanayemtaka.

Kamala Harris na Donald TrumpPicha: DW

Kwenye majimbo mengi, ikiwa mgombea ameshinda kwenye kura ya pamoja, anakuwa amewapata wachaguwaji wote. Kwa mfano, ikiwa Kamala Harris anashinda kura ya wengi ya jimbo la California, atapata kura zote 54 za wajumbe.Matokeo ya kwanza ya kura ya rais Marekani yatangazwa

Lakini majimbo ya Maine na Nebraska hayaruhusu wachaguwaji wake kuwa na nguvu za kumchaguwa mgombea mmoja kwenye kura ya jumla.

Kwenye majimbo hayo mawili, kura za wajumbe zinagawanywa kwa wagombea kwa mujibu wa kura ya jumla ilivyosema.

Ingawa katiba haiwalazimishi wajumbe kuwapigia kura wagombea waliopata kura nyingi kwenye majimbo yao, ni mara chache sana kwa wajumbe hao kwenda kinyume na matakwa ya wapigakura kwenye majimbo yao.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Usajili ya Marekani, "zaidi ya asilimia 99 ya wajumbe wamepiga kura kama walivyoahidi kwa wapigakura wao majimboni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW