1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Joachim Gauck aapishwa kuwa rais wa 11 wa Ujerumani

23 Machi 2012

Siku 5 baada ya kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Ujerumani,Joachim Gauck ameapishwa rasmi mbele ya wabunge wa mabaraza yote mawili,bunge la shirikisho Bundetag na baraza la wawakilishi wa majimbo Bunderat mjini Berlin.

Rais mpya wa Ujerumani, Joachim Gauck, anaapa mbele ya Spika wa Bunge.
Vereidigung Bundespräsident Joachim Gauck SchwurPicha: Reuters

Alikuwa spika wa bunge la shirikisho Bwana Norbert Lammert aliyefungua hafla hiyo maalum .Spika wa bunge amesema kuchaguliwa Gauck ni ushahidi wa maendeleo katika kukuwa pamoja wakaazi wa mashariki na magharibi ya Ujerumani.

Spika wa baraza la wawakilishi wa majimbo Bundesrat Horst Seehoffer amesema kuchaguliwa Joachim Gauck ni hatua muhimu katika historia ya Ujerumani."Mwanatheolojia wa Mashariki alikuwa mstari wa mbele katika mapinduzi ya amani ya mwaka 1989 katika Ujerumani mashariki ya zamani,amesema mwenekiti huyo wa chama cha kihafidhina cha CSU aliyeidaka kauli mbiu ya wakati ule "Wananchi ni sisi".

Baada ya sifa kwa rais mpya na shukurani kwa mchango wa mtangulizi wake Christian Wulff katika kuhimiza hali ya kuishi pamoja wananchi humu nchini,spika wa bunge la shirikisho Norbert Lammert alimkamatia rais mpya nakala ya katiba na kumuomba ale kiapo kuambatana na kifungu nambari 56 cha katiba:Joachim Gauck:

"Nnaapa kutumia nguvu na uweuzo wangu wote  kweaajili ya masilahi mema ya wananchi,kuwaepushia balaa kulinda sheria msingi na kanuni,kutekeleza kikamilifu jukumu nililopewa na kuhakikisha haki na usawa kwa wote.Mungu nisaidie"

'

Rais wa shirikisho Joachim Gauck anahutubia wajumbe bungeniPicha: Reuters

Mara baada ya kuapishwa rais mpya wa shirikisho Joachim Gauck amewasihi wananchi wawe na matumaini.Amesema wasi wasi  na hofu zinapunguza motisha na hali ya kujiamini.Ameitaja Ujerumani kuwa ni nchi ya miujiza ya demokrasia.

Rais wa shirikisho ameahidi kuhamasisha zaidi michango ya jamii."Wananchi wanaowajibika ndio wanaoimarisha demokrasia na kusawazisha ila.Wanchi ndio wanaopambana na maadui wa demokrasia na wafuasi wa siasa kali-amesistiza.

Rais Gauck ameahidi kuendeleza juhudi za mtangulizi wake katika kujumuishwa wahamiaji katika maisha ya kila siku ya jamii humu nchini."Wote wanaoishi humu nchini wanastahiki kujisikia nyumbani pia."Amesema rais Gauck.

Hadhara iliyoshiriki katika hafla ya kuapishwa rais mpyaPicha: Reuters

Mbali na wabunge sherehe hizo zimehudhuriwa pia marais wa zamani -Richard von Weizsäcker,Roman Herzog na Horst Köhler na pia mtangulizi wa Joachim Gauck Christian Wulff na mkewe Bettina.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/dpa/AFP/Reuters

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW