1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Biden amemfananisha Xi Jinping na viongozi 'madikteta'

21 Juni 2023

Rais Joe Biden wa Marekani amemfananisha mwenzake wa China Xi Jinping na viongozi "madikteta", matamshi yanayoweza kuzusha ukosoaji na upinzani mkali kutoka Beijing.

USA San Francisco Präsident Joe Biden
Picha: Susan Walsh/AP Photo/picture alliance

Akizungumza kwenye kikao na wafadhili wa chama cha Democratic huko kwenye jimbo la California, Biden amesema rais Xi alikasirishwa na uamuzi wa Marekani wa mwezi Februari wa kudungua puto kubwa la China ambalo Washington inadai lilitumika kufanya ujasusi.

China kujibu matamshi ya Biden

Amesema rais Xi hakuwa na taarifa juu ya uwepo wa puto hilo kwenye anga ya Marekani na kisa cha kudunguliwa kwake kilimfedhehesha kama ilivyo kwa viongozi madikteta ambao hukasirishwa pale wasipokuwa na taarifa juu ya masuala yanayotokea. China yumkini itajibu matamshi hayo ya Biden aliyoyatoa siku chache baada ya kukamilika kwa ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani mjini Beijing iliyolenga kupunguza mivutano baina ya nchi hizo mbili.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW