1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Joe Biden atangaza kuwania muhula wa pili wa urais

26 Aprili 2023

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kuwa atawania muhula wa pili katika uchaguzi wa mwaka 2024.

Irland, Ballina, | US Präsident Joe Biden
Picha: Leon Neal/Getty Images

Biden mwenye umri wa miaka 80 ndiye rais mzee aliyemo madarakani katika historia ya Marekani.

Biden amesema kila rika linakabiliwa na wasaa wa kusimama imara kwa ajili ya demokrasia na yeye anaamini kuwa wasaa huo sasa ni wa rika lake.

Pia ametamka kwenye ujumbe wa video kwamba inapasa kuimaliza kazi iliyoanzishwa. Rais Biden alitangaza uamuzi wake siku aliyotimiza miaka minne alipoanza kampeni yake ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Katika uchaguzi huo alimshinda rais wa chama cha Republican Donald Trump.

Chama cha Republican kimesema kwa uamuzi wa kuwania muhula wa pili rais Biden haoni alama za nyakati na kwamba wamarekani wanahesabu siku hadi hapo watakapomfungisha virago.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW