1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANESBURG. Wachimba migodi wafanya mgomo

8 Agosti 2005

Kwa mara ya kwanza katika miaka 18 wachimba migodi wa Afrika Kusini wameshiriki katika mgomo wa kudai nyongeza ya mishahara.

Mgomo huo umewahusisha takriban wachimba migodi 80,000 na habari zaidi zinaarifu kuwa huenda watu wengine 10,000 huende wakajiunga na mgomo huo baadae leo.

Mgomo huu umesababishwa na kutofaulu kwa mazungumzo baina ya kampuni nne za migodi na wawakilishi wa chama cha wachimba migodi cha Afrika Kusini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW