JOHANNESBERG:COSATU yaitisha mgomo wa kitaifa nchini Afrika Kusini
27 Juni 2005Matangazo
Jumuiya ya wafanyikazi nchini Afrika Kusini COSATU imesema huenda hii leo kukafanyika mgomo mkubwa wa wafanyikazi nchini humo.
Jumuiya hiyo imeitisha mgomo kote nchini dhidi ya ukosefu wa ajira pamoja na umaskini.
Maafisa wa jumuiya hiyo wamesema wafanyikazi wengi wanalipwa kiwango cha chini cha mshahara na kuendelezwa kwa taratibu za ubaguzi wa rangi
Idadi rasmi ya watu wasio na ajira nchini humo ni asilimia 25 lakini kwa mujibu wa jumuiya ya COSATU idadi hiyo imefikia takriban asilimia 40.