JOHANNESBURG. Makaazi ya Jacob Zuma yapekuliwa na maafisa wa Scorpion
19 Agosti 2005Maafisa wa kikosi cha kupambana na rushwa nchini Afrika Kusini Wemefanya msako kawenyed makaazi ya aliyekuwa makamu wa rasis Jacob Zuma ambae alitimuliwa kazini na rais Thabo Mbeki kwa shutuma za kupokea rushwa ya dola milioni 5 za ununuzi wa silaha.
Maafisa wa kikosi cha Scorpion walizipekua nyumba zote za bwana Zuma ya mjini na shamba na kuondoka na maboksi kadhaa.
Bwana Jacob Zuma atafika mbele ya mahakama mwezi oktoba kujibu mashataka ya rushwa.
Wafuasi wa bwana Zuma wameghadhabishwa na tukio hilo huku bwana Zuma mwenyewe akikanusha lawama zinazomkabili na kusema kwamba yeye ametolewa kama chambo katika siasa za Afrika ya Kusini.
Kufutwa kazi kwa bwana Zuma na kesi inayomkabili pamoja na kitendo cha uvamizi wa kikosi cha Scorpion yote haya yanatishia mgawanyiko katika muelekeo wa siasa zha Afrika Kusini.