1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG : Mandela asema kupambana na umaskini ni kitendo cha haki

3 Julai 2005

Shujaa dhidi ya ubaguzi wa rangi Nelson Mandela ametowa wito kwa viongozi wenye nguvu kubwa kabisa duniani kuzuwiya mauaji ya halaiki kwa kupambana na umaskini barani Afrika na kwamba kushindwa kufanya hivyo kutakuwa sawa na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini aliyatumia maonyesho ya muziki ya Johannesburg hapo jana kuwaonya viongozi wa mataifa ya magharibi kwamba historia itawahukumu kwa vitendo vyao.

Mandela amesema kuondokana na umaskini sio tu ni tendo la hisani bali ni kitendo cha haki na kwamba viongozi hao wa dunia wana nafasi ya kuandika historia kwa kufuta madeni,kuondowa vikwazo vya biashara visivyo vya haki na kuongeza msaada kwa Afrika.