1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG: Wachimba migodi waokolewa

10 Machi 2005

Timu ya wasaidizi nchini Afrika Kusini imefanikiwa kuwaokoa wachimba migodi wa mwisho walionasa ndani ya mgodi wa dhahabu baada ya mtetemeko wa ardhi kutokea katika eneo hilo.Wafanyakazi 40 kwa muda mrefu walinasa katika mgodi zaidi ya kilomita mbili chini ya ardhi.Maiti ya mfanyakazi mmoja aliefariki imeweza pia kutolewa.Nguvu za mtetemeko huo wa ardhi ulionyesha 5 kwenye kipimo cha Richter.Wataalamu wamesema hilo ni jambo lisilo la kawaida katika eneo hilo lililo kiasi ya kilomita 150 kusini-magharibi ya Johannesburg.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW